Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Maria Zakharova amesema, kwa kutumia madai ya mvutano uliopo baina ya Ukraine na Russia na tuhuma za nchi za Magharibi ikiwemo Marekani kwamba Moscow inapanga kuishambulia Kiev, nchi hizo za Magharibi zimo katika hali ya kuwapeleka nchini Ukraine wanamgambo waliopewa mafunzo ya kijeshi.
Zakharova ameashiria kuwa silaha na zana za kijeshi zenye thamani ya mabilioni ya dola zinamiminwa nchini Ukraine na kusema, suala hilo linahusiana na kupelekwa nchini Ukraine watu wenye silaha kwa kutumia anwani ya washauri.
Jumamosi iliyopita Rais Joe Biden wa Marekani alidai kuwa amemweleza Rais mwenzake wa Russia, Vladimir Putin, kwamba iwapo nchi yake itaishambulia Ukraine italipa gharama kubwa na kukabiliana na matatizo haribifu ya kiuchumi.
Biden alisema, suala la uwezekano wa kutumwa majeshi ya nchi kavu ya Marekani nchini Ukraine iwapo nchi hiyo itashambuliwa na Russia halijawahi kujadiliwa, japokuwa Washington na NATO zinalazimika kutuma majeshi zaidi kwa ajili ya kuimarisha nchi za Mashariki wanachama wa NATO.
Kwa wiki kadhaa, nchi za Magharibi zinazoongozwa na Marekani zimekuwa zikiishutumu Russia kuwa kupanga mashambulizi dhidi ya Ukraine kwa kutoa maoni yasiyo ya moja kwa moja kupitia ripoti za vyanzo vizivyojulikana.
342/